KITABU CHA FUNGUO NO2

HII NI BAADHI YA MAMBO YALIYOMO KATIKA KITABU CHANGU CHA FUNGUO NO2



KITABU HIKI NIMEAMUA KUKIANDIKA NA KUWEKA MAMBO MENGI HADHALANI ILI KUWAPUNGUZIENI TABU MBALI MBALI ZITOKANAZO NA UCHAWI NA MAJINI NA KILA AINA YA USHILIKINA.  MAANA BINADAMU WA SASA WAMEBADILIKA SANA NA HAWATAKI MAENDELEO YA WENZAO.
KWA MATATIZO YA MASHETANI NA MAJINI. ل WAGANGA MATAPELI HUTUMIA NJIA HII KUWAIBIA WATU, SASA NATOA ELIMU BURE NA NAMUOMBA ALLAH AWAFANYIE WEPESI DAWAZANGU ZIWASAIDIE NA MIMI PIA MUNIOMBEE NIZIDI KUWAPA ELIMU MBALI MBALI. AAMINA.       
                      YALIYOMO
(1)             Jinsi ya kujifungua kama umefungwa kichawi.
(2)             Jinsi ya kuvuta wateja katika biashara yako.
(3)             Jinsi ya kutoa mikosi mwilini.
(4)             Maajabu ya dua ya inna anzalnahu.
(5)             Dawa ya kuzuia chuma ulete.
(6)             Dawa ya kufukuza majini katika nyumba au mwilini.
(7)             Dalili za mtu mwenye majini na mashetani.
(8)             Dawa ya kuuzibiti unyumba au ndoa.
(9)             Dawa ya kutoa ulisho tumboni.
(10)       Dawa ya kumuona mwanga (mchawi)katika mji au biashara.
(11)       Dawa ya kumuosha mtoto alie athiliwa na kijasho.
(12)       Jinsi ya kuzuia mimba isipolomoke.
(13)       Dawa ya fahamu kwa mtoto wa shule.
(14)       Dawa ya kuongeza hisia kwa mke na mme.no2
(15)       Jinsi ya kupunguza unene.


JINSI YA KUJIFUNGUA KAMA RIZKIZAKO ZIMEFUNGWA KISHIRIKINA BIASHARA NK.
(1)             Chukua kindu saba usiku wakati unataka kulala kisha uzifunge fundo moja moja kisha unasema mimi nimefungwa kilakitu na alienifunga simjui sasa namimi nimejiongezea kifungo nafunga njia zangu pia nafunga ufalme wangu na nafunga nyota zangu hadi siku zitakapo fungua hizi kamba.  Kisha unaziweka mchagoni unalala na ikifika asubuhi unazitia ndani ya maji kwenyendoo ya kuogea weka na vifuatavyo.
(2)             Nazi moja.
(3)             Yai fresh moja.
(4)             Unga wa majani ya mbaazi.
(5)             Unga wa muosha fedha.
Oga hivyo vyote vikiwa ndani ya hiyo ndoo ya maji kisha unaanza kufungua kindu kwa kusema, alie nifunga alijua kamaliza sasa kuanzia sasa najifungua.
Ukimaliza kuzifungua uzichome moto halafu nazi na yai ni vya kuvuja kwa manuizi,
Unasema wewe yai umefungwa na sijui kama unamtoto wa kike au wa kiume namimi sijui akie nifunga  kama ni wa kike au ni wa kiume nitakavyo kufungua wewe yai namimi nifunguke haraka sana, unalivunja.
Kisha unakamata nazi unasema wewe nazi hufunga na kufungua namimi najifungua kuanzia sasahivi nafungua nyotayangu, nafungua ufalme wangu, nafungua biashara zangu, nafungua bahati zangu kwa uwezo wa muumba mbingu na ardhi.
Nnauhakika ukilifanya zoezi hili kwa ufasaha utaona ajabu ya mambo yatakavyo funguka na mambo yataenda vizuli.
Hii inatumika hata katika biashara unamwaga hizo dawa katika biashara kisha unafungua kwa mtindo huo huo.
Kabla ya yote mtangulize mwenyezi mungu utashinda kwa kila gumu litakua jepesi.

JINSI YA KUVUTA WATEJA KATIKA BIASHARA YAKO
Andika maneno haya katika karatasi nyeupe mala saba kwa kutumia dhafarani nyekudu na kimti cha kuandikia kiwe ki mti chochote ambacho utakikata sokoni au sehemu yoyote ya mkusanyiko wa watu.
Andika nenohili mara saba,( غلمش)
Kisha karatasi hiyo iwekee unga wa miski nyeupe, mchanga wa sokoni, na ubani zukra.
Karatasi hiyo unaifukiza ubani zukra wakatihuo unasema maneno yafuatayo,
Tawaqaru yaa khudama hadhihi ismu al adhim bihaqi daawat barahatii, utasema mala saba kisha unaenda kuizika njiapanda siku moja.
Ukisha itoa tayali kwa kuitundika katika biashara yako, utaona watu watakavyo ingia kama siafu kwa idhini ya allah.
Kumbuka kazihii utaifanya siku ya alhamisi mchana na utazika usiku wa kuamkia ijumaa.

Maoni

  1. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  2. Muosha fedha ni upi? Naomba ututumie hata picha

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi ya kujua nyota yako kwakutumia tarehe yako ya kuzaliwa

TAFSILI ZA NDOTO MBALI MBALI

TAREHE YAKO YA KUZALIWA NA MAANA YAKE.