TAFSILI ZA NDOTO MBALI MBALI

HIZI NI BAADHI YA NDOTO ZILIZOMO KATIKA KITABU CHANGU CHA NDOTO.

NDOTO
KILA NDOTO TUZIOTAZO HUA ZINA MAANA YAKE NA PIA NDOTO HUA ZIKO KATIKA MAKUNDI MATATU KUNA NDOTO ZA IBILISI, NDOTO ZA MWENYEZI MUNGU NA NDOTO ZA MAWAZO. PIA NDOTO ZIPO ZA UNABII AMBAZO WALIKUA WAKIOTA MANABII NA MITUME ENZI HIZO.
"KAMA MMOJA WENU AKIOTA NDOTO CHAFU NA MBAYA BASI ASIITANGAZE, MAANA NDOTO HIZO ZIMETOKA KWA SHETANI".
NA PIA NDOTO ZINAPATIKANA KATIKA BAIBO NA QORAANI
Dalili ni kutoka katika Qur'an 49:12
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ وَلا تَجَسَّسُوا وَلا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا
أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ
Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.
1. Mfano wa kwanza: Umeota umetumbukizwa kwenye Kisima, tafsiri yake ni surat Yusuf... Yaani Ndugu zako wanataka kukutendea uadui, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi mungu hawatafanikiwa wanavyotaka na utakuja kuwa na uwezo wa mali na mamlaka kuliko wao.
2. Mfano wa Pili: Umeota ndege amekudondoshea jiwe kichwani, Tafsiri yake Surat fil... Unaonywa kuwa unafanya yaliyovuka mipaka hivyo utaangamia.
3. Mfano wa tatu: Umeota Ndege anaokuambia kitu, Tafsiri yake ni surat Naml.. Habari anayokuambia ni ya kweli hivyo unatakiwa uifanyie kazi haraka.
4. Mfano wa nne: Umeota unakurupuka na ukaambiwa kiama!, watu wengi wanakwenda wasipopajua, Tafsiri yake ni kuwa unapewa Onyo kuna jambo linalomchukiza Mungu unalifanya acha mara moja. kumbuka pale allah aliposema kuwaambia waovu "Hakuna wanachokisubiri ila ni kiama ambacho kitawakuta Ghafla.
5. Ukiota katika ndoto kitu chochote chenye Ncha kali kama kisu, mkasi, panga, shoka, msumari sindano na jamii ya vitu hivyo ndoto hiyo inaashiria wewe uliyeota kupata habari mbaya za kifo, au kufungwa, ugonjwa,kufukuzwa kazi, kuibiwa, kutapeliwa, moto
6. Ukiota katika ndoto kitu chochote chenye kungara au cheupe, iwe nyumba gari, nguo, hiyo kwa muotaji ni dalili ya kupata “bahati nzuri au mambo mazuri.” Kupata pesa, kupata mchumba,safari yenye faida, kupata cheo, kupona mgonjwa,kuzaliwa mtoto
7. Ukiota katika ndoto kitu chochote kichafu au kisichopendeza, hiyo kwa muotaji ni dalili ya kupata upinzani na bahati mbaya. Kama kupingwa katika mambo yako, kufanyiwa fitna kazini au katika biashara, kutorokwa na mke au mpenzi, kupoteza mali, kuibiwa,kupigwa, kukamatwa au polisi kupata ajali.
8. Ukiota katika ndoto unapanda Juu kwa njia yoyote ile kama vile kupaa, kupanda ngazi kupanda kwa kamba, hiyo kwa muotaji ni dalili ya kupata mafanikio ya kimaisha, kadri unavyozidi kupanda ndio mafanikio yatakuwa zaidi.
9. Ukiota katika ndoto unashuka au unaanguka kwa njia yoyote ile, hiyo kwa muotaji ni dalili ya kukwama na kupata pingamizi katika mambo yako, kadri unavyozidi kwenda chini ndio kiwango cha kuharibikiwa kwa mambo yako.
10. Ndoto za kuota unastarehe zina maana tofauti ziko za bahati mbaya na zipo za bahati nzuri, kwa mfano ukiota unafurahia labda ngoma au harusi au tafrija au unacheza mziki uliokufurahisha, hiyo kwa muotaji itakuwa dalili ya mafanikio lakini kama ukiota uko katika sehemu hizo na hufurahi yale yanayoendelea hapo hiyo ni dalili ya kupata bahati mbaya.
11. Ndoto zingine zinatafsiriwa kulingana na mazingira mfano ukiota Kabati limejaa, maana yake mambo yako yatakuwa mazuri, kama pesa zitaongezeka, kama ugonjwa utapona, kama safari itakuwepo,kama kazi utpata cheo na kadhalika.
12. Kama ukiota kabati tupu maana yake mambo yako wewe muotaji yatakuwa mabaya.yote uliyonayo yatapotea, utaibiwa utatapeliwa, utaumwa na mengine mengi.
13. Kama ilivyo ndoto ya maji ukiota maji yametulia ni dalili ya mafanikio na bahati nzuri, utulivu wa mambokama ni kesi utashinda anayekudai atatulia na utawashinda maadui zako.
14. ukiota maji yenye mawimbi inaashiria ugumu wa mambo na matatizo. Utapata misukosuko ya kimapenzi, kikazi na kimaisha
15. Ukiota maji machafu, hiyo ni dalili ya bahati mbaya. Katika jambo lakololote unalotaka kufanya.
16. Ukiota Pingamizi katika ndoto mfano Ukuta, mlango, kufuli, dirisha, bonde, milima, au uzio, hizo ni dalili ya ugumu na upinzani katika mambo yako ambao utakumbana nao, mfano ukiota mlango ambao unafunguka kirahisi, hiyo ni dalili ya kupata upinzani mdogo, lakini ukiota mlango unafunguka kwa taabu, tegemea kupata pingamizi kali au ugumu mkubwa katika mambo yako.
17. Kuna ndoto zingine zinatafsiriwa kinyume, mfano ukiota Unalia maana yake utacheka au utapata hasara katika jambo lako lolote.
18. ukiota una woga basi utapata ujasiri.
19. ukiota umekuwa tajiri basi utapata umasikini.
20. Ukiota umepoteza, maana yake utapata.
21. Ukiota unakula nyama punguza kusengenya watu.Wengine ukiona wanakula nyama huenda wanakusengenya angaliakasorozako.
22. Ukiota unacheza karata= utapata bahati
23. Ukiota unakula kabeji= utapata maradhi ya kujitakia.
24. Ukiota unaona karanga= vulugu haziishi nyumbani.
25. Ukiota umevaa nguo mpya= utazawadiwa
26. Ukiota umevaa nguo nyeusi= utapata mikosi.
27. Ukiota umevua nguo= utapata hasala lakini kama nguohiyo ni cchafu= mikosi ita kuondoka.
28. Ukiota unavaa nguo zilizo chanika= utapatwa na aibu.
29. Ukiota umevaa nguo za mapambo au za maua= utapata furaha.
30. Ukiota unaendesha kigari cha farasi= utakua ombaomba.
31. Ukiota unachoma mkaa= utaoa mwanamke alie achika.
32. Ukiota umepata mafua= una maadui wa kisilisili.
33. Ukiota umeona mahindi= utapata faida katika shugurizako.
34. Ukiota uko kwenye ukumbi wa mziki = utapata habari nzuli toka kwa rafikiyako wa karibu.
35. Ukiota kiza kinene= utadanganywa au utatapeliwa.
36. Ukiota unaona giza kisha ukawa mwanga= kama ni mfungwa atafunguliwa na kama si mfungwa ni dalili ya mamboyako kufunguka.
37. Ukiota uko msibani= harusi. Ila ndotohii ikijirudia ni dalili ya jinni maiti.
38. Ukiota jinni limekudhulu au umeliogopa kupita kiasi= kuna hatali mbeleni.
39. Ukiota unachimba shimo na kisha likapotea= nidalili ya kukosa mazao na utafukuzwa kazi na pia ni dalili ya kukosa nvua.
40. Ukiota unatumbukia shimoni= utapata mikosi na utateseka sana ki maisha.
41. Ukiota unavuka mto kwa kutumia gogo= utapata watetezi katika mambo yako na kama unakesi utashinda kwa msaada wa mtu.
42. Ukiota umemuona dragon= utapata utajili kwa njia ya mazingara(madawa)
43. Ukiota umemuona chatu= utapata utajiri.
44. Mwanaume akiota anaona nguo ya kike imeanikwa= atapatwa na mabalaa.
45. Ukiota unakunywa maji wakati jua linachomoza na una kunywa kwa kutumia mkono wa kushoto= utapata maradhi.
46. Ukiota umelewa pombe kupita kiasi= utapata marafiki wa maana na pia ni mafanikio ki mapenzi.
47. Ukiota unazama ndani ya maji =nidalili ya kupata mikosi.
48. Ukiota unamuona mtu anazama ndani ya maji= mikosiyako itaisha.
49. Ukiota unaona funza= kaachonjo kuna maadui.
50. Ukiota unakula= mikosi.
51. Ukiota unalishwakitu= nikweli umelishwa.
52. Ukiota umekufa kwa kupigania dini= ama lizako ni njema.
53. Ukiota unakunywa maziwa= utapata mafanikio.
54. Ukiota mkeo matiti ni makubwa= utapata mafanikio.
55. Ukiota mbalamwezi inang”aa= utapata furaha na mafanikio
56. Ukiota umepotezapesa= utapata hasala ki biashara.
57. Ukiota umepatahela = mafanikio ila si kuokota.
58. Ukiota unaokotahela= utapata mikosi.
59. Ukiota umekunja chuma= umewashinda maadui.
60. Ukiota nyota inang”aa wakatihuo una mchumba= mtafarakana na mchumbawako.
61. Ukiota nyota imeanguka= afyanjema.
62. Ukiota umemuona bata mzinga= ndoa yenu ni ya mafanikio na mtapata watoto wengi.
63. Ukiota unang”okajino= utapoteza rafiki wa karibu.
64. Ukiota umeng”oka meno ya mbele utapoteza marafiki wengi na ndugu watakuchukia.
65. Ukiota unakunywa maji masafi= utapata furaha.
66. Ukiota unakunywa maji machafu= matatizo yanakunyemeleya.
67. Ukiota unaona maba= utapata maumivu.
68. Ukiota unachomwa mwiba= utapoteza pesa.
69. Ukiota radi inapiga= mafanikio katika biashara.
70. Ukiota radi imekupiga= umekumbwa na jinni.
71. Ukiota umemuona kobe= biashara zako zitaenda polepole
72. ukiota unakula kobe= mtalekebisha tofautizenu za ndoa.
73. Mwanamke alie achika akiota anafunga ndoa= ni mikosi.
74. Mgonjwa akiota anafunga ndoa na mwanamke alie achika= atakufa.
75. Ukiota unalia= ni fulaha na upendo.
76. Mgonjwa akiota anafunga ndoa na msichana ambae haja olewa= atapona,
77. Ukiota unaona karatasi nyeupe= utapata mke wa maana na watoto wa heli.
78. Ukiota unachana karatasi= utaendekeza umalaya.
79. Ukiota unatembea katika bara bara lililo nyooka= mafanikio mbeleyako na ni afya njema.
80. Mwanamme akiota anamuona tausi= atapata mke mzuri na atatajilika.
81. Mwanamke akiota anamuona tausi atapata mwanamme tajiri lakini ni muongo muongo.
82. Ukiota unamuona bundi= nimikosi na vifungo
83. Ukiota njegele zimepikwa= mafanikio.
84. Ukiota unakula mkaa= utapata mikosi na ni dalili ya kulishwa kitu.
85. Ukiota unaona vitunguu= utapata habali njema.
86. Mwanamme akiota anaona vitunguu= atapata mwanamke mwaminifu ila ni mwenye hasira.
87. Ukiota unachimba kaburi= jinni maiti na pia ni dalili ya kwa mba kuna tabia unayo ifanya si nzuli itakuingiza katika wakati mgumu.
88. Ukiota unalima na ng”ombe= mafanikio.
89. Ukiota watu wanalima na ng”ombe lakini zinazama= nidalili ya mavuno mabaya.
90. Ukiota watu wanalima juu ya mlima= utapoteza mifugo.
91. Ukiota umepewa tundadam chachu= utagombana na rafikiyako.
92. Tajiri akiota nasali= furaha
93. Maskini akiota anasali= matatizo na mikosi.
94. Mwanamme akiota anachota maji kisimani= ataoa.
95. Mwanamke akiota anachota maji kisimani= ataolewa.
96. Ukiota una kunywa wiski= ni mikosi, mabalaa, majuto.
97. Ukiota upepo wa kimbunga= utaoa mke mwenye makelele.
98. Tajili akiota amebemba mbao= mikosi
99. Maskini akiota amebeba mbao= bahati.
100. Ukiota una andika=jihadhari na kaulizako.
101. Ukiota unapiga miayo= rafikizako wamekuchoka.
102. Ukiota unaona kitu chochote cha njano= mafalakano katika mapenzi yenu.
103. Ukiota unamuona punda milia= kua mwangalifu katika maishayako.
104. Ukiota watu wanapiga talumbeta.= utapata mikosi na matatizo.
105. Ukiota unaona ndim= utapata ugonvi au kutukanwa.
106. Ukiota unaona mwanamke bikra= utapata habali njema.
107. Maskini akiota anatapika atapatapesa lakini kwa tajili atafilisika.
108. Ukiota vita= matatizo na huzuni.
109. Ukiota unamuona mamamkwe= utaugua.
110. Ukiota unaongeana mama yako vizuli= uta fanikiwa kwa lolote.
111. Ukiota mpishi yuko ndani ya nyumba= utaoa mwanamke wa maana na kama una matatizo. Yataondoka.
112. Mgonjwa akiota anamuona mpishi= haliyake itakua mbaya.
113. Ukiota unaona kisu= mafaninio.
114. Ukiota unamuona paka, utaibiwa.
115. Ukiota paka amekuuma= utaletewa habali za uongo.
116. Ukiota unakula keki= furaha na mafanikio.
117. Ukiota mshumaa unawaka kisha ukazimika= mamboyako yatahalibika pia ni ishala ya kufilisika.
118. Mgonjwa akiota mshumaa umewashwa = atapona.
119. Ukiota mshumaa ambao haujawashwa= utapata zawadi nono.
120. Ukiota unaona watoto wengi ndani ya nyumba= nidalili ya kufungika kwa kizazi.
121. Ukiota unakunywa kahawa= marafikizako ndo maaduizako.
122. Ukiota alie kufa anakwambia utakufa- huenda ikawa kweli.
123. ukiota mlango wa nyumba unaanguka, utaugua sana kisha utapona.
124. ukiota unafunga mlango wa nyumba yako, utampa talaka mke wako
125. Ukiuota msumari au daraja yako, Humaanisha mtu anayesaidia watu katika kutatua matatzo yao
126. Ukiota unapanda ngazi ya ubao au mota, Utapata hadhi kubwa duniani[cheo]kama katika ndoto kutakuwa na jambo la kuhashiria hali hii
127. Ukiota nyumba yako imeteketezwa, Utasumbuliwa na wenye mamlaka au ugonjwa wa mlipuko.
128. kuota mtu aliyekufa anakupa mawaidha au anakufundisha, Utapata wema katika dini yako kwa kiasi cha mawaidha yale.
129. kuota unamuoa mwanamke aliyekufa, unamuona kuwa yuko hai lakini kiuhalisia ameshakufa unamuoa na kuondoka nae ni ishara ya kuwa utafanya jambo litakalokufanya ujute.
130. kuota unafufuliwa, uwe peke yako au na wengine ni ishara ya kuwa wewe ni dhwaalimu.
131. kuota umeingia jehannam, Utafanya uchafu na madhambi makubwa,na kama umeota umeingizwa motoni basi yule atakayekuingiza atakupoteza na kukupelekea kwenye mambo machafu.
132. kumuota jini usingizini kimuona jini usingizini amesimama karibu na nyumba yako inakujulisha moja kati ya mambo matatu, 1.udhalili[unyonge], 2.hasara, 3.au nadhiri uliyoiweka.
133. Ukiota majini unawaona wameingia nyumbani kwako na kufanya mambo, Wezi wataingia nyumbani kwako na kukudhuru au maadui zako watavamia nyumba yako.
134. kumuota msichana amejipamba kiislam, Utaskia habari zitakazokufurahisha katika njia ambayo hukuitegemea.
135. ukimuota msichana yupo uchi, Utapata hasara katika biashara zako.
136. ukiota unachimba kaburi, Utapata hasara katika biashara zako Pia humaanisha utajenga nyumba.
137. kuuota ukuta , Kama utasimama juu ya kilele ni hadhi na nafasi yako kama utaporomoka utakuwa ni kiongozi wa uharibifu.
138. ukiota unauza nyumba yako, Kufikia kikomo cha maisha yake.
139. ukiota una beba mlima, Utabebebshwa mizigo mikubwa na watu wakorofi na wakali.
140. kuota unapanda kuelekea sehemu ya juu, Muotaji atapata heshima,atatukuzwa na kupanda cheo.
141. kuota miamba na mawe, Ugumu wa moyo,ukorofi,ukatili na kibri.
142. kuota changarawe, Usengenyaji na kutoa shutuma dhidi ya mtu Fulani.
143. kuota mchanga,vumbi au udongo unakurukia au anakula, Utakuwa tajiri jitume sana katika kazi zako.
144. unatembea juu ya mchanga au kuokota mchanga, Utafanya kazi ngumu za sulubu ili kuwa na mali.
145. mchanga au vumbi kuruka hewani au mbinguni, Mambo ya muotaji yatavurugika
146. kumuota mtoto wa kiume, Ni adui dhaifu ambaye atakujia kwa kudhihirisha urafiki kisha atadhihirisha uadui wake.
147. ukiota kwenu kumezaliwa watoto wengi wa kiume, Ni dalili ya majonzi na huzuni.
148. kumuota bibi kizee, Akiwa amejipamba na amaejifunua~utapata dunia yako na biashara za haraka akiwaAmekunja uso~kuondoka kwa darja ya juu kwa mambo yako ya kidunia , Ana sura mbaya~mambo yako yatageuka, yupo uchii~ ni dalili ya kufedheheka.
149. ukiota uso wako ni mweusi kuliko sehemu zingine za mwili
150. kuota umekatwa shingo kwa upanga, Mkeo atazaa mtot wa kike.
151. Ukiota Kichwa chako kimetengana na mwili ni ishara ya kuwa kama mgonjwa utapona,una deni utalipa,utahiji,kama una vita utapata faraja.kama unamjua aliyekukata hivyo vyote vitapitia kwake.
152. mwanamke kuota umenyolewa, Ni ishara ya kifo au utaachwa.
153. mwanamke akiota amenyolewa na mumewe, Mumewe atamfungia nyumbani kwake kwani hakika ndege hubakia kiotani wakati amenyonyolewa mbawa zake.
154. ukiota unasikiliza kwa macho na kuona kwa masikio, Utampelekea binti yako au mkeo kufanya maasi.
155. ukiota kiganja chako kina jicho au nyama, Utapata mali.
156. Ukiota panya anatoka nje anaingia ndani, mkeo ni mzinifu.
157. Ukiota umeokota au unacheza na funguo matarajio ni utapata neema.
158. .Kuota mwili umekosa nguvu/kama umepooza: Katika ndoto hii ni kweli mtu hujisikia kama mwili umepooza wakati akiota na hiyo humaanisha kuwa mtu huyo amepoteza control katika maisha yake.
159. .Kuota unaanguka: Hii inaweza kumaanisha kuwa mambo katika maisha yako hayaendi vizuri. Inaweza kuwa kazini, uhusiano au masuala ya fedha.
160. .Meno: Kuota umetoka meno kunamaanisha kuwa una uoga wa kujiona hauna mvuto na inaweza kuhusiana na hisia ya kujiona umefedheheshwa na kitu maisha mwako.
161. 5. Kuota Unakimbizwa: Utakuwa unaepuka hisia inayokutisha ama ikuumizayo, mtu ama jambo fulani baya.
162. 8.Kuota Maji: Kunamaanisha mabadiliko au vitu vipya. Inaweza kumaanisha pia kuhusu kubadilika mambo/vitu katika maisha yako.
163. . Kuota vyombo vya usafiri: Ndoto hizi huonesha muelekeo ambao maisha yanatupeleka.
164. Ukiota unajisaidia haja ndogo inamaanisha utaondokewa na matatizo madogomadogo.
165. kuanguka kisimani, Utakumbwa na huzuni na masikitiko mwishowe utapata furaha.
166. kuzama baharini , Kama maji ni safi ni ishara utazama katika mambo ya utawala na serikali, kama ni maji chumvi na yana taka utapata taabu itakayokusababishia kuangamia.
167. Ukiota kunguru itatafsirika kama mtu fisadi na asiyekuwa na haya.
168. Ukiota kizingiti cha mlango kimetoka, tafsiri yake ni mwanamke wako atakutoloka.
169. Ukiota ubavu wako umechomoza, tafsiri yake ni mwanamke wako atakutoloka.
170. Ukiota unakula majani, utakula mtaji wa biashara yako.
171. Ukiota unakula mkaa, utapata maradhi ya tumbo.
172. Ukiota unauza mkaa, uta filisika.
173. Ukiota unaingiliwa kinyume na maumbile, adui yako atakushinda.
174. Ukiota wewe unafanya namme mwenzio kinyume na maumbile, nidalili ya kumshinda adui.
175. Ukiota mala kwa mala misiba, una majini wachafu.
176. Ukiota unapigana na ukapaa, kuna uadui unakunyemelea au kuna wanga wanakuwangia lakini una viumbe wanao kusaidia.
177. Ukiota visiki vingi viko njiani, kunawatu wanao kwamisha mipango yako.
178. Ukiota unakula nyama ya mtu, wewe ni msengenyaji.
179. Ukiota unapigana na radi kisha ukaishinda, kuna jinni alitaka kukuingia lakini kashindwa.
180. Ukiota unakabwa, huyo ni jinamizi lakini anae kukaba ukimjua huyo ni mwanga.
KAMA HUJA ELEWA PIGA 0767 393934 AU 0657 555550

Maoni

  1. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  2. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  3. Mm nimeota nimetumbikia ktk maji machafu Lkn sikuzama kuna MTU akaja kunvuta mkono nkatoka

    JibuFuta
  4. Nimeota nime jifnya chizi nkaingia kwenye dimbwi la maji machafu nakutok maana yake nini

    JibuFuta
  5. Nimeona Nimekuota hela kwenye ndoto lakini ndani ya ndoto hiyo nimepata changamoto nyingi sana pamoja na misukosuko. Ila baadae mambo yakawa sawa. Hii ina maana gani

    JibuFuta
  6. ukiota unamuua nge (scorpion) nini maana yake

    JibuFuta
  7. Nimeota meteor shower / kwa luga yetu ni VIMONDO vingi sana vinaruka tena vina ng'aa sana ,maana yake ni nini ??

    JibuFuta
  8. Je ukiotta unajisaia hajakubwa maana yake nin

    JibuFuta
  9. Nmeota Nina mimba n niko clinic hii ndoto imerud mara ya pili hii manake nini?

    JibuFuta
  10. Naomba nisaidie maana ya hii nimeota nimepotea njia yani nimehangaika sana hadi kuikuta njia sahihi, mpaka naikuta njia sahihi nimehangaika nimepita kwenye tope nimelowa chepechepe to

    JibuFuta
  11. Ukiota unanyonyesha mtoto mchanga

    JibuFuta
  12. Ukiota Kinyonga yuko na watoto wake..,maake nini..?

    JibuFuta
  13. nimeota napanda sehem mlimani ila nikawa nashindwa baadae akatokea mtu akanipa ngazi nikapanda mpaka juu nikaenda nyumbani kulala wakati nimelala nikaskia sauti ikiniita kwa jina la nyumbani kuwa niamke napigwa na kweli nikapigwa na kitu kama mbao nikashtuka na kuanza kusali hiyo ilikuwa saa 8 by saa9 nikapata usingizi tena nikalala lakini pia mtu huyohuyo akarudi kama ananichezea nywele kichwani nikaamka tena japo kwenye ndoto nakumbuka nilimkwangua na kucha so nikaomba tena nikalala lkn saa 10 tena niliamka baada ya huyo mtu kurudi kunisumbua ndotoni. kwa kumbukumbu ya ndoto ni mwanaume

    NOTE: ndoto hiyo nimeota nikiwa naona mazigira ya chumbani kwangu na neti aliyofungua kuja kunipiga na hicho kitu ni neti ambayo ninayo chumani kwani so mazingira ni yale ninayo ishi.. nilikosa usingizi mpka asubuhi.

    JibuFuta
    Majibu
    1. Dada Hafsa najua ni muda mrefu sasa tangu ulupoandika comment hii, sasa sijui u hali gani, ila ntafte kwa namba hizi niongee Zaidi na wewe, plz fanya hvyo 0742422328. 0715 276 940.0620138150

      Futa
  14. nyota yangu nimezaliwa 14june naomba nijue nyoya yangu

    JibuFuta
  15. Nimeota nipo sokoni ila soko alina watu kuna watu kama watatu tuu na ikachinjwa kondoo nipewe

    JibuFuta
  16. Nimeota nimepakiwa kwenye pikipiki nanyeshewa mvua kisha aliyenipakia akaniacha ikiwa naendelea kunyeshewa, wakati huohuo nikaota mwembe umekatika ambao embe nyingi ni changa, lakini nikaokota moja iliyoiva.

    JibuFuta
  17. M nimeota mke wangu ananiomba tuachane m na mm nikawanambembeleza lakini akagoma

    JibuFuta
  18. Nimeota tumevamiwa na mwanamke ila baadae nikafanya mapenzi na yule mwanamke na kisha nikaondoka naye kwaajili ya kwenda kufanya naye mapenzi, wakati narudi kambini nikajikuta nimepotea, katika kubangaika kutafuta njia nikawa nipo ufukweni nikaogelea kwenda ng'ambo nilipofika kule pia hapakuwa kambini nikaanza kuogelea tena kutudi lakini nikiwa nimechoka sana pia sikuona kama nilifanikiwa kurudi kambini

    JibuFuta
  19. Kama upande wa jicho la chini linacheza maana take nn

    JibuFuta
  20. Nimeota nakimbizwa namkichaa tena ameshika kisu kila mtaa akiniona ananifuata na kisu je inamaana gani..?na nifanyeje?

    JibuFuta
  21. Ukiota umeona tu jeneza nn maanabyake

    JibuFuta
  22. Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
    Anasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
    *Kama unataka kupata mimba.
    *Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
    *Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
    *Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
    *Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
    *Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
    Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi ya kujua nyota yako kwakutumia tarehe yako ya kuzaliwa

TAREHE YAKO YA KUZALIWA NA MAANA YAKE.